top of page
KENYA NEWS HEAD_edited.jpg

Serikali imeahidi kuanzisha maonyesho madogo madogo ya vitabu ili kuunga mkono juhudi za wadau mbali mbali katika kukuza na kuendeleza utamaduni wa kujisomea kwa watanzania lakini pia kuongeza upatikanaji wa vitabu mashuleni kwa bei rahisi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Mosses Nnauye (Mb.) wakati wa Hafla ya ufunguzi rasmi wa maonyesho ya uuzaji wa vitabu yaliyofanyika leo katika ukumbi wa diamond jubilee jijino dar es salaam na kubainisha kuwa mainyesho hayo yana tija chanya kwa taasisi za elimu na watanzania kwa ujumlahususa ni katika kubadilisha mtazamo kuhusu umuhimu wa kusoma vitabu ili kuongeza maarifa na ujuzi kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo.

 

Kwa upande mwingine mshauri wa kampuni ya uchapishaji vitabu ya sharjah publishing city na mwakilishi wa kampuni ya big bad wolf mohamed hersi amewashukuru wadau waliojitokeza kwenye maonyesho hayo na kuahidi kuwa vitabu hivyo vimezingatia maadili bora ya mtanzania na pia maonyesho hayo yatakidhi mahitaji ya wote watakaojitokeza hivyo amewataka kuendelea kujitokeza kwa wingi.

 

Nae mmoja wa waliohudhuria maonyesho hayo ameelezea umuhimu wa maonyesho hayo kwa watanzania na kuhimiza watu kujitokeza kwa wingi kujipatia vitabu hivyo vinavyohusu nyanja mbalimbali katika jamii ili kukuza na kuongeza wigo wa usomaji wa vitabu

 

Maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya diamond jubilee yanatarajiwa kudumu kwa siku kumi na yatafikia tamati mnamo tarehe 18 septemba mwaka huu.

Maonyesho ya vitabu yafana Dar, Waziri Nape atoa neno.

10 SEPT 2022

KENYA

bottom of page